Alhamisi, 9 Aprili 2015
BABU SEYA KUACHIWA HURU NA RAIS KIKWETE
Kwa mujibu wa KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977, SURA YA PILI, SEHEMU YA KWANZA, IBARA YA 45, inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, ama bila ya masharti au kwa masharti, au kumwachilia kabisa mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote.
Nguza na mwanaye Papii walitoa ombi la kusamehewa na kuachiwa huru kupitia wimbo wakati wakitumbuiza katika maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Chuo cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam tar 20/06/2014.
Ombi hilo waliliwasilisha kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambapo Babu Seya na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha), walitumbuiza wakiwa na Bendi ya Wafungwa. Walimwomba Waziri Chikawe kufikisha ombi lao kwa Rais Kikwete. Chikawe akijibu ombi hilo alisema “Mtu akishatumikia kifungo kwa miaka
Jumatano, 8 Aprili 2015
JESHI LA KENYA LIMEFANYA MASHAMBULIZI KWA KIKUNDI CHA ALSHABAAB SOMALIA
Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab
katika taifa jirani la Somalia ,msemaji wa jeshi ameiambia BBC.
Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo, linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza. Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya. Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo. Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki iliopita. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi. Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya jumapili usiku katika eneo hilo. Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.

Jumanne, 7 Aprili 2015
MAMA MZAZI NA MWANAE WAPEWA MIMBA NA MWANAUME MMOJA
Mwanaume mmoja aitwaye Vincente Malumane amewatandika mimba mama na mtoto wake na wote kujifungua mwezi mmoja, hii imetokea Afrika Kusini.Imeelezwa kuwa mama huyo aliyefamika kwa jina la Mildred Mashego, alichukizwa baada ya kuujua ukweli huo, japo anasema anamchukia Vincente kwa kumchanganya yeye na binti yake ila hana kinyongo chochote na mtoto wake na hivi sasa yeye na mwanae wanawalea watoto wao pamoja, hofu waliyonayo kwa sasa ni jinsi ambavyo watawaelezea watoto wao watakapokua wakubali.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)